Mlemavu
wa ngozi Damas Valeniani aliyecharangwa mapanga na mfanyabiashara
maarufu mkoani Morogoro anayefahamika kwa jina moja la Lyimo.
Jamaa huyo maarufu kwa jina la Mangi, anadaiwa kutenda unyama huo wiki
iliyopita usiku wa manane kwenye Msitu wa Milima ya Uluguru, Mtaa wa
Bingwa Kiwasi Juu, Kilakala, wakati mlemavu huyo, akiwa amelala.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, mlemavu huyo alisema:
“Nilikuwa nimelala, ghafla nikasikia mtu akiingia akiwa ameshika panga na kuanza kunikatakata huku akitaka kuninyofoa masikio yangu. Nilimtambua kuwa ni Lyimo ambaye ni jirani yetu.”
“Nilikuwa nimelala, ghafla nikasikia mtu akiingia akiwa ameshika panga na kuanza kunikatakata huku akitaka kuninyofoa masikio yangu. Nilimtambua kuwa ni Lyimo ambaye ni jirani yetu.”
Alisema kuwa baada ya kuona hali hiyo, alijitetea vya kutosha na
kufanikiwa kuchomoka, kwa bahati nzuri mpwa wake, Mathias John alitokea
na kumsaidia huku wakipiga kelele za kuomba msaada lakini tayari alikuwa
amshamcharanga panga kichwani na kusababisha atokwe na damu nyingi.
Alisema kuwa kutokana na woga alioupata, aliogopa kulala hivyo alikimbilia kwa mjumbe wa mtaa wao, Filemon Gyuna ambako alipatiwa huduma ya kwanza.
Alisema kuwa kutokana na woga alioupata, aliogopa kulala hivyo alikimbilia kwa mjumbe wa mtaa wao, Filemon Gyuna ambako alipatiwa huduma ya kwanza.
“Kulipokucha ndipo tukaenda kuripoti polisi na kupewa jalada la kesi namba MOR/RB/5122/2014-SHAMBULIZI.
“Polisi walifika nyumbani na kumkamata mtuhumiwa na kumfikisha kwenye
mkono wa sheria na mimi nikapewa PF-3 kwa ajili ya matibabu kwenye
Hospitali ya Mkoa wa Morogoro,” alisema Damas kwa maumivu makali.
Akihojiwa na mwandishi wetu juu ya tukio hilo, mwenyekiti wa mtaa huo,
Ally Malekela alikiri kutokea kwa tukio hilo na kueleza kwamba Lyimo
alipewa saa 24 za kuhama kwenye mtaa huo.
Wananchi mbalimbali waliozungumza na Ijumaa Wikienda, walisema Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, SAC Leonard Paul, anatakiwa kufanya kazi
ya ziada ili kukabiliana na matukio kama hayo.
Kwa upande wake, mwenyekiti wa Chama cha Maalbino Mkoa wa Morogoro, David Mganga alisema: “Natoa wito kwa jamii ielewe kuwa kiungo cha albino hakiwezi kumpa mtu utajiri au mafanikio, waache kututesa sisi maalbino.”

0 comments:
Post a Comment