Aug 17, 2014

Wanigeria 85 wakombolewa kutoka Boko Haram

Vikosi vya Chad vimewakomboa Wanigeria 85 waliokuwa wametekwa nyara wiki iliyopita na wanamgambo wa kundi la Boko Haram huko kaskazini mashariki mwa Nigeria. 
Afisa wa Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Taifa (NHRC) huko Maiduguri makao makuu ya Jimbo la Borno amesema kuwa, wanaume 62 na wanawake 22 wamekombolewa huku wengine 30 bado wametekewa nyara na kundi hilo.

 Agosti 20 wanamgambo wa Boko Haram walivamia kijiji cha Doron Baga katika pwani ya ziwa Chad na kuwateka nyara wanaume 100 na wanawake kadhaa.

 Watu wasiopungua 28 waliuawa na nyumba kadhaa kuchomwa moto katika shambulizi hilo.

Watu hao wamekombolewa baada ya msafara wa wanamgambo wa Boko Haram kusimama katika mpaka wa Chad ambapo ulitiliwa shaka.

0 comments:

Post a Comment