Machafuko yameendelea Marekani katika mji wa Ferguson,
Missouri baada ya vikosi vya usalama kuwashambulia waandamanaji ambao
wanalalamikia hatua ya polisi mzungu kumpiga risasi na kumuua kijana
mweusi au Mwafrika Mmarekani.
Kijana huyo hakuwa na silaha yoyote wakati
wa kupigwa risasi.
Ikumbukwe kuwa Agosti tisa, Michael Brown mwenye
umri wa miaka 18 alipigwa risasi kadhaa na kuuawa na polisi katika mtaa
wa St. Louis mjini Ferguson.
Tokea mauaji hayo ya kibaguzi yajiri
kumekuwepo na maandamano kila usiku katika mji huo ambao wakaazi wake
wengi ni Wamarekani weusi.
Maandamano dhidi ya ubaguzi wa rangi yameripotiwa katika
miji mingi kote Marekani.
Jana Jumaposi kumeripotiwa mapambano mitaani
baina ya polisi na wananchi waliokuwa na hasira.
Polisi wa kuzima ghasia
waliokuwa na silaha nzito nzito na magari ya deraya walitumia mkono wa
chumba kukabiliana na waandamanaji.
Maandamano pia yalifanyika
Washington DC nje ya Ikulu ya White House ambapo washiriki wamelaani
vikali ukatili wa polisi katika kukabiliana na waandamanaji.
Rais Obama
wa Marekani ametoa wito wa utulivu na amewataka polisi waheshimu
waandamanaji na wachunguze mauaji ya kijana huyo.
Pamoja na Marekani
kudai ni kinara wa haki za binaadamu lakini vikosi vya usalama nchini
humo vinalaumiwa kwa kutekeleza mauaji ya kibaguzi dhidi ya watu wasio
na hatia hasa Wamarekani wenye asilia ya Kiafrika.
0 comments:
Post a Comment