Aug 6, 2014

' Anti Balaka wamekiuka makubaliano ya amani CAR'

Magaidi wa Anti-Balaka  
Magaidi wa Anti-Balaka
 
Msemaji wa Mungano wa Seleka katika Jamhuri ya Afrika ya Kati amesema kuwa, hatua ya kundi la Kikristo la Anti Balaka ya kuyaunga mkono majeshi ya Ufaransa dhidi ya wanamgambo wa Seleka inakinzana na makubaliano ya amani yaliyofikiwa hivi karibuni huko Brazzaville, Jamhuri ya Kongo.

Djouma Narkoyo amesema kuwa, majeshi ya Ufaransa yakipata uungaji mkono wa Anti Balaka yalifanya mashambulio dhidi ya wanamgambo wa Seleka na kuua wapiganaji wasiopungua 50 huko kaskazini mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati. 

Taarifa zinasema kuwa, mapigano hayo yamejiri masaa machache tu baada ya Andre Nzapayeke Waziri Mkuu wa nchi hiyo kujiuzulu wadhifa huo. 
Wakati huohuo, Rais Catherine Samba –Panza wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ameanza kufanya mazungumzo na wawakilishi wa makundi mbalimbali kwa lengo la kumteua Waziri Mkuu mpya wa serikali ya mpito. Rais Samba –Panza ameeleza matumaini yake kwamba, Waziri Mkuu mpya atachaguliwa kufikia wiki ijayo.

0 comments:

Post a Comment