Jul 6, 2014

SHEIKH Qardhawi apinga 'Khilafa' ya Daesh Iraq

Msomi wa Misri mwenye makao yake Qatar Sheikh Yusuf Qardhawi ametangaza kupinga tangazo la matakfiri wa Daesh la kuanzisha kile wanachokiita ni 'Khilafa' au utawala wa Kiislamu katika maeneo waliyoyateka Iraq.
Qardhawi aliyeunga mkono magaidi hao wa Daesh huko Syria sasa amesema Daesh ni tishio kwa madhehebu ya Sunni na kwamba 'Khilafa' iliyoanzishwa ni batili kwa mtazamo wa sheria za Kiislamu. 

 Qardhawi ambaye ni mashuhuri kama 'Shekhe wa Fitna' kutokana na uungaji mkono wake kwa makundi yenye misimamo mikali amesema: "Sisi tuna matumaini kuwa  Ukhalifa utarejea katika nchi za Kiislamu.

 Hatahivyo harakati za kundi linalojiita Dola la Kiislamu Iraq na Sham yaani Daesh zitakuwa na matokeo mabaya katika maisha ya Ahle Sunna nchini Iraq na 'Mapinduzi ya Syria'. 

Ameongeza kuwa, kutangaza kuundwa 'Khilafa ya Kiislamu' ni hatua yenye misimamo mikali yenye lengo la kujipatia umashuhuri tu na wala haitakuwa na msaada wowote kwa Uislamu. 

Amesema cheo cha 'Khalifa wa Kiislamu' si cheo cha kundi maalumu na kwamba Waislamu wote wanapaswa kushirikishwa katika uundwaji dola la Kiislamu.

0 comments:

Post a Comment