Jul 6, 2014

Matakfiri wa Daesh wabomoa misikiti Iraq

Ziara la Sheikh Ahmed ar Rifa'i-eneo la Mahlabiya nje ya Mosul likibomolewa na magaidi wa Daesh Ziara la Sheikh Ahmed ar Rifa'i-eneo la Mahlabiya nje ya Mosul likibomolewa na magaidi wa Daesh
Magaidi wa kitakfiri kutoka kundi linalojiita Dola la Kiislamu la Iraq na Sham (Daesh) wamebomoa misikiti na maeneo kadhaa matakatifu ya Waislamu wa madhehebu ya Shia na  Sunni katika mkoa unaokumbwa na vita wa Nainawa nchini Iraq.
Taswira za video zilizotolewa na magaidi hao wa kitakfiri zinaonyesha wakitumia mabuldoza kubomoa maziara ya masharifu wa Kisuni sambamba na kumbomoa misikiti ya Mashia. 

Taarifa zenye kusikitisha zinasema kuwa magaidi hao wa kitakfiri wamebomoa maziara manne ya viongozi wa tariqa za Kisunni huku wakibomoa misikiti sita ya mashia. 

Aidha matakfiri hao wamekalia kwa mabavu makanisa mawili ya Wakristo wa pote la Orthodox na kuvunja misalaba na kuweka bendera zao sehemu yake.

 Yote hayo yamejiri ndani ya mji wa Mosul na nje kidogo ya mji huo ulio kaskazini mwa Iraq. 

Magaidi hao wa kitakfiri pia wametoa taarifa kadhaa wakisema watabomoa maeneo yote matakaktifu ya kidini na kihistoria kote Iraq. 

Kundi hilo la Daesh linalaumiwa kuyavunjia heshima matukufu ya kidini katika maeneo mbali mbali ya Iraq. 

Inaaminika kuwa magaidi wa Daesh wanapata uungaji mkono wa mashirika ya kijasusi ya Saudi Arabia na Qatar na pia himaya isiyo ya moja kwa moja ya utawala haramu wa Israel.
 

0 comments:

Post a Comment