Jul 3, 2014

Raia 82 wauawa kwenye mapigano mapya CAR

Waziri wa Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Aristide Sokambi amesema kuwa, kwa akali watu 82 wameuawa kwenye mapigano mapya yaliyotokea hivi karibuni katika mji wa Bambari ulioko katikati mwa nchi hiyo.
Waziri Sokambi ameyasema hayo jana baada ya kutembelea mji huo na kusisitiza kwamba, nyumba zisizopungua 176 pia zimebomolewa na kuteketezwa kwa moto. 

Waziri wa Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amefanya safari hiyo kwa lengo la kupata takwimu halisi za maafa yaliyosababishwa na mapigano yaliyotokea hivi karibuni mjini humo. 

Mapigano hayo yameugawa mji wa Bambari katika sehemu mbili, moja ikiwa ya Waislamu na sehemu nyingine Wakristo.

Kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, mapigano yamekuwa yakiendelea katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na wahanga wakubwa wa machafuko hayo ni Waislamu ambao wamekuwa wakiuawa kiholela na wanamgambo wa Kikristo wa Anti Balaka.

0 comments:

Post a Comment