Jul 3, 2014

Pata taarifa namna BALOZI wa Libya nchini Tanzania alivyo jiua


BALOZI wa Libya nchini Tanzania amejiua kwa kujipiga risasi kichwani.


Taarifa zilizowasilishwa kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam zinajuza  kuwa balozi huyo kwa jina Ismail Nwairat, alijipiga risasi Jumanne usiku na kufariki akiwa anapokea matibabu hospitalini.

Msemaji wa serikali ya Tanzania Arthur Mwambene amethibitisha taarifa hiyo kuwa balozi huyo alijiua ndani ya makao ya ubalozi wa Libya mjini Dar es Salaam Jumanne usiku.

0 comments:

Post a Comment