Jul 6, 2014

Nyumba za Waislamu zateketezwa moto Myanmar

Waislamu katika eneo hilo wanalaumu polisi kwa kutochukua hatua zozote wakati genge la magaidi wa Kibudha lilipovamia mtaa wa Waislamu na kuteketeza moto shule na majengo mengine ya Waislamu jana Jumamosi.
Walioshuhudia wanasema maafisa 70 wa polisi walikuwa wakitazamaji tu wakati Mabudhaa walipokuwa wakitekeleza jinai hiyo dhidi ya Waislamu. 

Hujuma hiyo ilijiri punde tu baada ya mazishi ya Mbudha aliyepoteza maisha katika machafuko yaliyojiri mjini humo hivi karibuni. 

Julai pili katika mji huo wa Mandalay, watawa wa Kibudha waliwaua Waislamu wawili na kuwajeruhi wengine 14. Maelfu ya Waislamu wya kabila la Rohingya wameuawa nchini Myanmar katika miaka ya hivi karibuni kufuatia hujuma za Mabudha wenye misimamo mikali nchini humo.

Makumi ya maelfu ya Waislamu wamelazimika kuacha makazi yao nchini na kukimbilia usalama katika nchi jirani. 

Waislamu wa kabila la Rohingya ni karibu asilimia tano ya watu wote sitini milioni nchini Myanmar lakini pamoja na hayo wamekuwa wakikandamizwa, kudhulumiwa na kuteswa tokea nchi hiyo ipata uhuru wake mwaka 1948. 

Umoja wa Mataifa unasema Waislamu wa kabila la Rohingya katika jimbo la Rakhine nchini Myanmar ni kati ya watu wanaodhulumiwa zaidi duniani.

0 comments:

Post a Comment