Jul 6, 2014

Magaidi wanaharibu jina la Uislamu duniani


Ayatullah Hashemi Rafsanjani  
Ayatullah Hashemi Rafsanjani

Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu Iran amesema lengo la magaidi katika jinai zao zilizo dhidi ya ubinaadamu ni kuharibu sura ya Uislamu duniani.

Ayatullah Hashemi Rafssanjani aliyasema hayo jana mjini Tehran alipokutana na Hussein Sadiqi balozi wa Iran nchini Saudi Arabia. 

Rafsanjani amesema magaidi wanatumia kisingizio cha kupinga baadhi ya serikali za nchi za mabara ya Afrika na Asia ili kuharibu sura ya Uislamu duniani na kwa njia hiyo wanahalalisha jinai zinazotendwa na Wazayuni. 

Ayatullah Rafsanjani ameashiria nafasi ya Iran na Saudi Arabia katika ulimwengu wa Kiislamu na mfumo wa kimataifa na kusema: "Ili kukabiliana na misimamo mikali na kuzuia kuenea tena ujahili, kuna udharura wa kuwepo juhudi za pamoja za nchi za Kiislamu hasa Iran na Saudia ili kuondoa dhana kuwa nchi za Kiislamu zinahitaji madola ya kigeni kulinda usalama wao.

" Ayatullah Rafsanjani amesema Maulamaa wa Kiislamu hasa Iran na Saudi Arabia wanapaswa kuchukua jukumu muhimu la kuwaita Waislamu kuelekea katika msimamo wa wastani, umoja, udugu na amali njema ili taswira halisi ya Uislamu iwasilishwe duniani.

0 comments:

Post a Comment