Hausigeli aliyedaiwa kuteswa na mtuhumiwa huyoMwanamke
Yasinta Rwechengura, mkazi wa Boko wilayani Kinondoni, Dar
anayekabiliwa na kesi ya kutuhumiwa kumtesa hausigeli wake kwa miaka
miwili (siku 730), amejikuta akihenyeshwa mahakamani.Hayo yamemkuta juzi
alipofikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya
Kinondoni kujibu tuhuma zinazomkabili ambapo alikuwa akipokea amri
kutoka kwa askari na kumfanya kukosa raha.
Msala
huo unagusa hisia za wengi ndiyo maana watu kutoka viunga mbalimbali
vya Jiji la Dar walifurika mahakamani hapo kusikiliza mwenendo wa kesi
hiyo iliyosomwa mbele ya Hakimu Mkazi, Boniphace Lihamwike.
Akisoma
kesi hiyo mahakamani hapo, wakili wa serikali ambaye alikuwa upande
wa jamhuri, Mohamed Salum alisema anaiomba mahakama hiyo kutotoa dhamana
kwa mtuhumiwa kwa sababu za kiusalama.
Sababu ya pili alisema bado hali ya mgonjwa ni mbaya na amelazwa kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Kesi
hiyo ambayo inafuatiliwa kwa ukaribu na wanaharakati wa haki za
binadamu, awali ilikuwa inasikilizwa na Hakimu Suleiman Mzava ambaye
juzi hakufika mahakamani hapo kutokana na uhamisho alioupata na badala
yake kesi hiyo ilitajwa kwa Hakimu Lihamwike.
Upande
unaomtetea mtuhumiwa huyo uliokuwa ukiongozwa na wakili wa kujitegemea,
Msomi Gidion, uliiomba mahakama kumpa mteja wao dhamana lakini ukagonga
mwamba.
Hata hivyo, wakili Mohamed aliendelea kuiomba mahakama kwa mara nyingine kutotoa dhamana kwa mtuhumiwa kwa sababu alizozitoa awali.
Hata hivyo, wakili Mohamed aliendelea kuiomba mahakama kwa mara nyingine kutotoa dhamana kwa mtuhumiwa kwa sababu alizozitoa awali.
Hakimu
aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, alisema pande zote zilikuwa na hoja
akianza na upande wa mtuhumiwa ambapo alitoa ufafanuzi kuwa ni haki
yake ya kikatiba kupata dhamana lakini upande wa jamhuri nao ulikuwa na
hoja.
Hakimu
huyo alisema kuwa shauri hilo kwa mara ya kwanza lilianzia kwa hakimu
mwingine na ndani ya faili la kesi hiyo hakukuwa na vielelezo vyovyote
hivyo kuirudisha kesi hiyo kwa hakimu kiongozi kwa ajili ya kupangiwa
hakimu atakayeisikiliza.
Baada
ya hapo, mtuhumiwa alipandishwa kwenye karandinga na kurudishwa
mahabusu kwenye Gereza la Segerea, Dar kuendelea kuhenya hadi
atakapopata dhamana huku wananchi waliofika mahakamani hapo
wakimshangaa.
HABARI NA PICHA KWA HISANI YA GP
0 comments:
Post a Comment