Jul 6, 2014

Majibizano ya risasi yasikika Pwani ya Kenya


Pwani ya Kenya hivi karibuni ilikubwa na mauaji ya zaidi ya watu 60 na kutishia hali ya usalama katika eneo hilo
Pwani ya Kenya hivi karibuni ilikubwa na mauaji ya zaidi ya watu 60 na kutishia hali ya usalama katika eneo hilo

Kumesikika majibizano ya risasi katika Pwani ya Kenya jumamosi jioni katika eneo ambalo takribani watu 60 waliuawa mwezi uliopita,mamlaka imethibitisha.

Kitengo cha kushughulikia majanga kiliarifu kupitia mtandao wa twita kuwa kulitokea majibizano ya risasi katika kituo cha biashara jirani na mji wa Mpeketoni palipotokea mauaji.

Kitengo hicho kimesema mamlaka za ndani na polisi walionyesha ushirikiano wa haraka kudhibiti usalama katika eneo hilo na hakuna watu walioathiriwa na tukio hilo.

Nalo shirika la msalaba mwekundu la kenya limesema hakuna waathirika katika tukio hilo.

Tukio hilo limetokea katika eneo mashuhuri kufikiwa na watalii takribani kilo mita 15 kutoka Lamu.

0 comments:

Post a Comment