Madaktari wa Ukanda wa Ghaza katika hospitali ya
Shuhadaaul- Aqsa wamefanikiwa kuokoa maisha ya mtoto mchanga ambaye
mimba yake ilikuwa na umri wa miezi nane na nusu kutoka katika tumbo la
mama aliyeuawa shahidi kwa hujuma ya ndege za kivita za utawala haramu
wa Israel katika ukanda huo.
Kwa mujibu wa kanali ya televisheni ya
al-Alam, mtoto huyo aliokolewa baada ya kugundulika kuwa alikuwa angali
hai ndani ya tumbo la mama yake, licha ya kwamba mama yake mzazi alikuwa
amekwishafariki dunia.
Habari zaidi zinasema kuwa ndege aina ya F 16 ya
utawala haramu wa Israel iliishambulia nyumba aliyokuwa akiishi Shaimaa
na Ibrahim (wazazi wa mtoto huyo) na kumuua shahidi Shaimaa huku Bwana
Ibrahim akijeruhiwa vibaya katika hujuma hiyo.
Inaelezwa kuwa baada ya
shambulizi hilo, mama wa mtoto huyo aliangukiwa na vifusi vya nyumba
iliyokuwa imeharibiwa vibaya.
Juhudi za waokoaji zilifanikisha kumuondoa
mama wa mtoto huyo ambaye wakati huo tayari alikuwa ameuawa shahidi
huku mtoto akionekana kuwa hai suala lililowafanya kuuharakisha mwili wa
mzazi huyo katika hospitali na kufanikiwa kuokoa maisha ya kichanga
hicho.
0 comments:
Post a Comment