Jul 28, 2014

Mufti wa Daesh aangamizwa kaskazini mwa Iraq

Jeshi la Iraq limetangaza kuwa limemuua mufti wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu Iraq na Sham katika mji wa Huwaija, katika mkoa wa Kirkuk, kaskazini mwa nchi hiyo. 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, baada ya jeshi hilo kugundua maficho ya sheikh huyo wa kundi hilo la kitakfiri anayejulikana kwa jina la Dandah al-Halabi, lilianza kufuatilia nyendo zake na kufanikiwa kumkuta katika msikiti wa Quddus wa mji huo wa Huwaija ambapo ameuawa yeye na watu wengine sita waliokuwa wakiandamana naye.
Kabla ya hapo Dandah alikuwa sheikh wa kundi la kigaidi la Jab'hatu Nusra la Syria na baada ya kuachana na kundi hilo alijiunga na kundi la Daesh na kuingia Iraq.

Kwa mujibu wa jeshi la Iraq, sheikh huyo wa Kisalafi alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu, kutokana na fatwa zake za kupotosha jamii. 

Kwengineko jeshi la Iraq, limewaangamiza wapiganaji 50 wa kundi hilo akiwemo kiongozi mwandamizi anayejulikana kwa jina la Abu Shukr as-Suri, mjini Tikrit. 

Jeshi la Iraq pia limeteketeza zaidi ya magairi 15 yaliyokuwa yakitumiwa na kundi hilo.

0 comments:

Post a Comment