Jeshi la Iraq limeua makumi ya wanamgambo wa kundi la kitakfiri
linalojiita Dola la Kiislamu nchini Iraq na Sham (Daesh) wakiwemo raia
wa Saudia na Chechnya katika operesheni kadhaa. Ripoti rasmi iliyotolewa
na jeshi la Iraq, inasema kuwa, magaidi wapatao 82 wameuawa katika
mashambulizi ya anga katika viunga vya kaskazini mwa mkoa wa Salahud Din
nchini Iraq. Wanamgambo wengine wameuawa katika mashambulizi ya anga
kaskazini mwa mji wa Baaquba ambayo yameangamiza pia magari yaliyokuwa
yamebeba idadi kadhaa ya wanamgambo wa kundi hilo.
Awali viongozi wandamizi wa kundi la Daesh waliuawa katika mashambulizi ya ndege wakati walipokuwa wamekusanyika katika moja ya bustani za eneo la al-Abd kaskazini magharibi mwa mji wa Hillah ambapo wengi wao walikuwa na uraia wa Saudia na Chechnya.
Mbali na hayo jeshi la Iraq pia limeyasafisha maeneo mengi ya mji wa Diyala kutokana na uwepo wa magaidi.
Kwengineko, kanali ya televisheni ya al-Arabiyyah ya Saudia, imetangaza leo kuwa, serikali ya nchi hiyo imeweka katika mipaka ya pamoja na Iraq askari wake 3,000.
Huku hayo yakiripotiwa jana Waziri Mkuu wa Iraq, Nour al Maliki alitoa msamaha dhidi ya makundi ambayo yamekuwa yakipigana dhidi ya serikali yake miongoni mwa watu wa makabila tofauti ya nchi hiyo.

0 comments:
Post a Comment