Jul 2, 2014

Ikhwanul Muslimin walaani hujuma mjini Cairo

Hujuma nje ya Ikulu ya Rais, Cairo Juni 30 2014 Hujuma nje ya Ikulu ya Rais, Cairo Juni 30 2014
 
Harakati ya Ikhwanul Muslimin nchini Misri imelaani vikali mashambulizi ya  jana nchini humo. Mashambulizi hayo yalitokea jana karibu na ikulu ya rais wa nchi hiyo ya al-Ittihaadiyyah na kupelekea askari wawili kuuawa.
Aidha mashambulizi hayo matatu yametokea sambamba na kuanza kwa kumbukumbu ya maandamano ya tarehe 30 Juni, maandamano yaliyopelekea kuondolewa madarakani kwa nguvu aliyekuwa rais wa nchi hiyo Muhammad Morsi. 

Mbali na askari wawili kuuawa, wengine pia wamejeruhiwa vibaya katika shambulizi hilo. Hadi sasa hakuna kundi lolote lililotangaza kuhusika na tukio hilo. 

Wakati huo huo idara ya usalama nchini humo imetangaza kuwatia mbaroni watu sita wanaodhaniwa kuwa walihusika katika mashambulizi hayo. 

Awali maafisa wa usalama wa Misri walikuwa wametangaza kuwa, wahusika wa tukio hilo si raia wa nchi hiyo. 

Muhammad Ibrahim, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Misri amesema kuwa, vitendo vya aina hiyo kamwe haviwezi kuvunja irada na azma ya serikali mpya ya taifa hilo.

0 comments:

Post a Comment