Jul 2, 2014

Gaza yahujumiwa baada ya mauaji ya vijana wa kiyahudi

 Ndege za Israel zimeyashambulia maeneo ya Wapalestina katika ukanda wa Gaza,baada ya kupatikana miili ya vijana 3 waliotekwa nyara Juni 12. Israel inawashutumu Hamas kuhusika na matukio yote mawili dhidi ya vijana hao.

Opereshini za kijeshi za Israel zimepamba moto Chama cha Hamas kinakanusha kuhusika na utekaji nyara pamoja na mauaji ya vijana hao watatu wa kiume ambapo wawili - Gil-Ad Shaer na Naftali Fraenkel aliyekuwa na uraia wa Marekani na Israel, wote walikuwa na umri wa miaka 16 na mwengine Eyal Yifrah miaka 19. 

Wakati Israel imekula kiapo kwamba mauaji hayo hayatapita hivi hivi, bali dola hiyo ya Kiyahudi itahakikisha wahusika wanakamatwa 

, Hamas imeonya kuwa hatua yoyote ya Israel kushambulia itakuwa na athari zisizotabirika .
 
Taarifa ya Hamas pia imekuja wakati ndege za kivita za Israel zikiyapiga maeneo 34 ndani ya Gaza , tukio linalofuatia shambulizi la maroketi 18 la wapalestina ndani ya ardhi ya Israel katika mpaka wake wa kusini.

Katika kikao cha baraza la mawaziri kuhusu usalama, jeshi kupitia waziri wa ulinzi lilipendekeza hatua za wastani dhidi ya wapiganaji katika Ukingo wa magharibi, lakini maafisa walisema hakuna maafikiano yaliopatikana na kwamba kikao hicho kitaendelea. 

wasi wasi uliopo miongoni mwa wanaotahadharisha juu ya hatua kali za kijeshi ni kuwa huenda hilo likahujumu mamlaka ya Rais Mahmoud Abbas anayeungwa mkono na Marekani.

Israel inamtaka Mahmoud Abbas asishirikiane na Hamas
Mkuu wa chama cha Hamas,Khaled Meshaal
Hata hivyo msemaji wa Waziri mkuu Netanyahu , Mark Regev aliitaka mamlaka ya utawala wa Palestina isitishe ushirikiano na Hamas, aliyowaita kuwa magaidi.

"Nafikiri kutokana na uovu huu, haya mauaji ya kikatili ya vijana hawa wakiume, hapana budi mamlaka ya palestina yasitishe muungano wake na Hamas. 

kiongozi wa palestina rais Abbas hawezi kusema wanaheshimu amani na maridhiano na wakti huo huo, kuwa katika ushirika wa kisiasa na magaidi hawa- wauaji hawa wa watoto."

Kwa upande mwengine waziri mkuu wa Israel Netanyahu amekitumia kisa cha vijana hao watatu kumtaka rais Abbas aufute mkataba wa maridhiano na Hamas, ambacho ni hasimu wake mkubwa. 

Mapatano hayo yalifikiwa mwezi Aprili na kufungua njia ya kuundwa serikali ya umoja ya wapalestina Juni 2.

Kauli za kulaani mauaji ya vijana hao watatu wakiisraili, zimetolewa na rais Barack Obama wa Marekani, waziri mkuu wa Uingereza David Cameron na Papa Francis Kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki duniani .

Wakati kitisho cha hali ya wasiwasi kikizidi kutanda katika eneo hilo, afisa mmoja wa kibalozi wa kiarabu mwenye uzoefu na harakati za upatanishi zinazofanywa na Misri, katika mgogoro wa Israel na Palestina- akinukuu taarifa ya Marekani alisema mjini Cairo kwamba anatarajia serikali ya Netanyahu itaifuatialia hali hii kwa tahadhari.

Mwanabalozi huyo alisema , " sifikiri kama Israel iko tayari kubadili msimamo.

 Inaweza kuwaadhibu wale waliohusika na uhalifu huu, lakini isivuke mpaka na kuwahujumu raia ambao hawahusiki nauhalifu huo.

Kamata kamata inaendelea katika maeneo ya utawala wa ndani
Watu wanaomboleza baada ya kupata habari ya kuuliwa vijana watatu wa kiyahudi waliotekwa nyara Juni 12 iliyopita

Kwa upande mwengine,msemaji wa jeshi la Israel alisema wanajeshi walifyatua risasi dhidi ya mtu mmoja aliyetambuliwa na wapalestina kwa jina la Yousouf Al-zagha mwenye umri wa miaka 19, ambaye aliwatupia wanajeshi hao bomu la mkono, wakati walipojaribu kumkamata mpiganaji mmoja katika kambi ya wakimbizi ya Jenin. 

Lakini mpalestina mmoja aliyeshuhudia alisema Zagha alikua mpita njia tu asiye na hatia.

Baada ya miili yao kupatikana juzi jioni,Vijana watatu wakiume wakiisraili waliotekwa nyara na kuuwawa na tukio hilo kuwa chanzo cha hali hii ya wasiwasi ya hivi sasa, walizikwa jana.

0 comments:

Post a Comment