Apr 23, 2014

Uganda yamtia mbaroni kamanda wa LRA huko CAR

Wanajeshi wa Uganda wamemtia nguvuni afisa wa Kundi la Wanamgambo wa Kikristo wa LRA na kuwakomboa mateka kumi.

 Msemaji wa jeshi la Uganda Paddy Ankunda ameeleza kuwa afisa huyo wa LRA kwa jina la Charles Okello amepelekwa rumande huko kusini mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Ankunda amemtaja  Okello kuwa ni kamanda wa kivita wa kundi la Kikristo lenye sifa mbaya  la LRA na kuongeza kuwa kilicho muhimu ni kuwa, wamewakomboa watu kumi, ambao ni watoto saba na wanawake watatu, waliokuwa wakishikiliwa mateka na LRA kwa muda wa miezi sita.

Itafahamika kuwa, jeshi la Uganda limekuwa likiongoza kikosi cha Umoja wa Afrika kilichopewa jukumu la kuwasaka na kuwatia nguvuni wanachama wa LRA, huku baadhi yao wakisakwa kwa udi na uvumba na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) ya mjini the Hague Uholanzi.  


0 comments:

Post a Comment