Apr 9, 2014

TUZIUNGE MKONO TAASISI CHANGA ZA KIISLAM



 MUSTWAFA ABDUL MURO
0754 710 241
MKURUGENZI MKUU WA LINKSOFT COMMUNICATION SYSTEMS.
Waislamu nchini wametakiwa kuziunga mkono taasisi changa za kiislamu ili ziweze kuzitumikia vyema jamii.

Wito huo umetolewa hivi karibuni na Mustwafa Abdul Muro alipokutana na viongozi wa Munira Madrasa iliyopo Magomeni Makuti Jijini Dar es salaam.

Katika mazungumzo hayo maalumu yaliyofanyika katika ofisi za Madrasa hiyo,Bwana muro akiwa kaambatana na Bwana Yahya R.Mgaya alisema "kwa kweli nimeridhishwa sana na utendaji wenu,na nina sema mumekaba kila idara"

"Hii itanifanya mbali ya mimi kuwaunga mkono lakini pia nikawashawishi ndugu,jamaa na rafiki zangu ili wawaunge mkono katika harakati zenu za maendeleo,kwani muna haki ya kuungwa mkono"alisema.

"Katika hali ya kimazoea ni ngumu sana kuamini kwamba madrasa inaweza kuleta maendeleo hasa yanayokwenda sambamba na teknolojia iliyopo ulimwenguni hivi sasa,lakini nyinyi munira munaonekana mumepiga hatua na kama watu watawaunga mkono,mutafika mbali sana"alisema.

Akizungumzia taasisi ya munira kuwa na mtandao wa blog alisema "vijana wengi wamezama katika internet,kwa bahati mbaya sana wengi wao wanakutana na mambo mabaya yenye kuwapoteza na hii ni kwa sababu wengi wao hawajui kama ipo mitandao inayoweza kuwapatia habari zenye muelekeo mzuri"

"Unajuwa wataalamu wanasema internet ni sawa sawa na barabara kubwa ambayo inasafirishwa bidhaa za kila aina,iwe mbaya au bidhaa mzuri,sasa matunda utakayo yapata yatatokana na namna wewe utakavyoitumia"mwisho wa kumnukuu bwana muro ambaye ni mkurugenzi mkuu wa Linkosoft Communication Systems.

Awali Ustaadh Juma Rashid ambaye ni katibu mkuu wa Munira Madrasa alimtambulisha Bwana Muro kuwa mbali ya taasisi hiyo kujitahidi kuisaida jamii kwa kiasi kidogo kinachotokana na michango ya wapenda kheri,lakini pia taasisi hiyo inatoa elimu kwa njia mbali mbali ikiwemo ya ufundishaji wa darasani,semina,mihadhara,maigizo,vijarida na utunzi wa vitabu.

Aliongeza kwa kusema wamezindua mtandao wa blog kwa lengo la kuelimisha na kuhabarisha.

"Kwa sasa tunajiandaa kwa tamasha kubwa la elimu kwa wanafunzi wa Madrasa za kata ya Magomeni,litakaloanza tarehe 29/05/2014 hadi tarehe 31/05/2014 In Shaa Allah,ambapo jumla ya shilingi milioni 6,738,500/ zinahitajika"alisema Ustaadh Juma Rashid.

0 comments:

Post a Comment