Mjumbe wa Bunge la Katiba, Zitto Kabwe
amesema kuandikwa kwa Katiba isiyokubaliwa na pande zote kutasababisha
gharama kubwa kuliko zile zinazotajwa za serikali tatu.
Akichangia hoja
kwenye Bunge hilo jana, Zitto alisema kuna kila sababu ya kukaa na
kukubaliana ili kupata Katiba itakayokubalika pande zote.
“Muundo
wa Muungano una hatari ya kuvunjika iwapo hakuna matakwa ya dhati ya
watu kuungana... Maneno ya kusema Serikali tatu zitavunja Muungano ni ya
siasa na hayana msingi wa kisayansi.
Urusi ilivunjika sababu haikuwa na
demokrasia na siyo sababu ya idadi ya Serikali,” alisema.
Zitto
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali
(PAC), alisema hofu ya gharama inayotajwa katika uendeshaji wa muundo wa
serikali tatu haina msingi wowote kwa kuwa hakuna ushahidi wa kitaalamu
unaothibitisha gharama hizo.
“Nimesikia watu wanasema eti
tutalazimika kujenga ikulu mpya, nani kasema lazima tuwe na marais
watatu? Tunaweza kuwa na rais mmoja kwenye nchi na wakuu wa nchi
washirika wawili… Ni jambo la makubaliano tu,” alisema.
Alisema
bajeti ya mwaka huu ni Sh18 trilioni, kati ya hizo Sh5.3 trilioni ndizo
zinazohudumia wizara za Muungano, lakini serikali ina uwezo wa
kukusanya kodi zaidi ya Sh10 trilioni pamoja na mapato mengine.
“Kuna
jumla ya Sh2.3 trilioni hatuzikusanywi kila mwaka kutoka kwenye kampuni
kubwa, kwa uwezo wetu wa pato la ndani asilimia 17 tunao uwezo wa
kuendesha serikali ya muundo wa idadi yoyote.
“Hofu ya
Serikali ya Muungano kutokuwa na fedha ni sababu halisi, ni kweli kwamba
ushuru wa bidhaa pekee yake hauwezi kutuendeshea serikali. Sasa nini
kazi yetu, tunaingia hapa ili kuboresha hayo maeneo, kama hatuwezi
tumekuja kufanya nini hapa?” alihoji.
Jussa ashambulia
Mjumbe
wa Bunge hilo, Ismail Jussa jana alisisitiza kwamba Wazanzibari wengi
hawapo tayari kuendelea na mfumo wa serikali mbili kwa sababu unawatesa
na kuwadhalilisha.
Jussa ambaye ni mjumbe wa Baraza la
Wawakilishi Zanzibar kupitia CUF, alisema haoni haya kuzungumzia suala
hilo kwa niaba ya Wazanzibari.
“Hoja nyingi zimetoka (kuhusu
Muungano), lakini naendelea kuzungumza kwa niaba ya wananchi wa
Zanzibar na katika hili sioni haya kwa sababu naamini kwamba
wanakisimamia kile ambacho sisi tunasimamia nacho ni Zanzibar yenye
mamlaka kamili,” alisema Jussa
Apr 17, 2014
KATIBA ISIYORIDHIWA NA WANANCHI,ITATUGHARIMU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment