Mar 2, 2014

Jihadul Islami yataka kutekwa askari wa Kizayuni

Kiongozi mwandamizi wa harakati ya Jihadul Islami ya Palestina amesema kuwa, kutekwa nyara askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel ndio njia bora zaidi itakayosaidia kuachiliwa huru maelfu ya wafungwa na mahabusu wa Kipalestina wanaoshikiliwa kwenye jela za utawala huo ghasibu. 

Akizungumza kwenye mkutano wa kuwaunga mkono wafungwa wanaogomea  kula na wagonjwa wa Kipalestina  wanaoshikiliwa kwenye jela za Israel, Khadhwar Habib amesisitiza kuwa, njia pekee na bora zaidi itakayosaidia kukombolewa maelfu ya wafungwa hao wa Kipalestina ni kushikiliwa mateka askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel. 

Khadhwar Habib ameongeza kuwa, mpango wa kuendelezwa mazungumzo kati ya Wapalestina na Wazayuni yenye shabaha ya kuachiliwa huru wafungwa hao hauna faida yoyote kwa Wapalestina. 

Kiongozi huyo mwandamizi wa Jihadul Islami amesisitiza kuwa, Wapalestina wasitegemee kabisa kuachiliwa huru idadi kubwa ya wafungwa wa Kipalestina kwa njia ya mazungumzo, kwani utawala ghasibu wa Israel bado unaendeleza siasa zake za ukandamizaji dhidi ya wafungwa hao. 

Khadhwar Habib ameutaka ulimwengu wa Kiislamu na Kiarabu kutekeleza majukumu yake ipasavyo kuhusiana na wafungwa wa Kipalestina.

0 comments:

Post a Comment