CHAMA cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), kimesema ripoti ya
utafiti wa ukatili wa udhalilishaji wa kijinsia inaonesha Zanzibar
inaongoza kwa matukio ya ukatili wa kijinsi.
Utafiti huo umeonesha idadi ya wasichana wanaoolewa wakiwa na umri mdogo wa kati ya miaka 15 hadi 19 nchini ni asilimia 2.8.
Akizungumza na wanahabari Dar es Salaam juzi, Mjumbe wa Bodi ya
TAMWA, Gladness Munuo, alisema mafaniko ya utafiti huo Zanzibar
yametokana na wahusika kuwa wawazi katika kutoa taarifa zinazowahusu
tofauti na Tanzania Bara ambako kumekuwa na urasimu.
“Lengo la utafiti huu lilikuwa ni kuangalia kiwango cha matukio ya
ukatili wa kijinsia katika wilaya 14 za Tanzania Bara na sita za
Zanzibar,” alisema.
“Utafiti ulijikita katika maeneo ya ubakaji, ukeketaji, vipigo,
kutelekezwa wanawake na watoto, mauaji ya vikongwe, ndoa na mimba za
utotoni,”alisema.
Alibainisha kuwa utafiti huo ulifanywa na wanahabari kwa muda wa siku 10
na kwamba umethibitisha bila Tanzania bado ina kiwango kikubwa cha
ukatili wa kijinsia.
Alisema matukio yaliyobainika wakati wa utafiti ni pamoja na ndoa za
utotoni, kuozwa kabla hawajajitambua, wanawake kupigwa na kutukanwa,
wanaume kutekeleza familia, ndoa za mitala, vipigo na mauaji
Feb 22, 2014
Zanzibar yaongoza kuripoti udhalilishaji
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment