Feb 22, 2014

Maelfu ya raia wa CAR wakimbilia Cameroon


Makumi ya maelfu ya raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wamekimbilia nchi jirani ya Cameroon tangu mwanzoni mwa mwezi huu wa Februari kufuatia kushadidi machafuko huko Jamhuri ya Afrika ya Kati. 

Kamisheni Kuu ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa imetoa ripoti ikieleza kuwa raia elfu 28 kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati wamekimbilia Cameroon.
Dan Mac Norton, msemaji wa Kamisheni Kuu ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa amesema kuwa, wakimbizi hao wako katika hali mbaya sana na kwamba wengi wao wana uhaba wa chakula na hawana mahali pazuri pa kuishi. 

Jamhuri ya Afrika ya Kati ilikumbwa na machafuko na ukosefu wa amani baada ya kuingia madarakani Rais Michel Djotodia mwishoni mwa mwaka jana. 

Machafuko na mauaji dhidi ya Waislamu yangali yanaendelea licha ya kuweko vikosi vya kimataifa khususan wanajeshi wa Ufaransa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati.

0 comments:

Post a Comment