Rais wa Uganda Yoweri Kaguta
Museveni amesema kuwa anataka kuwapa fursa wanasayansi kuchunguza iwapo
hisia za watu wa jinsia moja husababishwa na maumbile ama tabia kabla ya
kuamua kuutia sahihi au la mswada tata wa watu wa jinsia moja.
Mswada huo uliowasilishwa bungeni mnamo mwaka 2009 awali ulipendekeza hukumu ya kifo kwa watu wa jinsia hiyo,lakini badala yake ukafanyiwa marekebisho ya kuhudumia kifungo cha jela kwa watakaopatikana na hatia.
Marekani imeonya kuwa uhusiano kati yake na Uganda utaharibika iwapo rais Museveni atatia sahihi mswada huo.
Rais Museveni amesema kuwa wanasayansi nchini Uganda watafanya utafiti huku akiwataka wanasayansi wa marekani kusaidia katika uchunguzi huo.
Waandishi wanasema rais huyo anajaribu kuwafurahisha watu wenye misimamo ya kadri mbali na kutoharibu uhusiano wake na mataifa ya magharibi ambayo ni wafadhili wakubwa wa taifa hilo.
0 comments:
Post a Comment