Eneo la Ikulu ya Somaliaambalo kundi la wanamgambo la Alshabab lilishambulia
Ikulu ya Mogadishu nchini Somalia imerejea kwenye umiliki wa vikosi vya
Serikali, kufuatia mashambulizi ya makomandoo wa Al-Shabab waliojaribu
kuvamia ikulu ya rais.
Waziri wa ulinzi wa Somalia, Abdikarim Hussein Guled
amewaambia wanahabari mjini Mogadishu kuwa baada ya saa kadhaa za
makabiliano kati ya vikosi vya Serikali na wanamgambo hao wamefanikiwa
kuwafurusha na kuilinda Ikulu ya rais Hassan Sheikh Mohamud.
Wanamgambo wa Al-Shabab walitumia magari kujitoa muhanga na kurusha maroketi kwenye Ikulu lakini hawakufanikiwa kuingia ndani, kufuatia ulinzi mkali uliopo kwenye Ikulu ya Mogadishu.
Umoja wa Mataifa UN umesema kuwa rais, Hassan Sheikh Mohamud hakujeruhiwa kwenye shambulio hilo, ambalo ni kubwa zaidi kuwahi kufanywa na wanamgambo hao kulenga Ikulu ya Mogadishu.

0 comments:
Post a Comment