Mahakama moja ya Kenya imeanza kusikiliza kesi ya watu 70
wanaokabiliwa na tuhuma za ugaidi na ambao walitiwa mbaroni kufuatia
vurugu za hivi karibuni za Masjid Musa mjini Mombasa.
Washukiwa hao walifikishwa mbele ya Hakimu Mkuu Mwandamizi katika Mahakama ya Mombasa, Richard Odenyo ambapo walikana mashtaka yote yanayowakabili ikiwa ni pamoja na ugaidi, wizi wa kutumia mabavu, kumiliki silaha kinyume cha sheria na uchochezi. Wakili wa washukiwa hao, Mohammad Balala, ametaka waachiliwe kwa dhamana lakini upande wa mashtaka umepinga ombi hilo na kuwataja kuwa ni tishio kwa usalama. Watabakia korokoroni hadi Februari 26 wakati uamuzi utakapochukuliwa kuhusu ombi lao la kutaka kuachiliwa kwa dhamana. Washukiwa hao walitiwa mbaroni Februari 2 mwezi huu wakati polisi walipouvamia Msikiti wa Musa mjini Mombasa kutokana na kile walichosema ni ripoti kuwa vijana Waislamu walikuwa wanatayarishwa kwa ajili ya kufanya mashambulizi ya kigaidi.
Wakuu wa Polisi ya Kenya wanadai kuwa baada ya kuuvamia msikiti huo walipata bunduki aina ya AK 47, risasi, visu na bendera za kundi la kigaidi la al Shabaab lenye ufungamano na mtandao wa al Qaeda.
Hujuma ya msikiti huo imeibua mgawanyiko katika safu za viongozi wa Kiislamu nchini Kenya huku baadhi wakiunga mkono hatua ya polisi na wengine wakipinga.
Serikali ya Kenya imesema itachukua hatua kali kukabiliana na wanaotumia maeneo ya ibada kueneza misimamo mikali ya kidini.

0 comments:
Post a Comment