Waandamanaji wapiga kambi mji kiev Licha ya rais Yanukovych kutangaza kufikia makubaliano na upinzani
Maelfu ya waandamanaji wameendelea kusalia mjini Kiev licha
ya mpango uliokusudiwa kumaliza mzozo wa kisiasa nchini Ukraine ambao
watu kadhaa wamepoteza maisha.
Mpango uliosainiwa ijumaa kati ya raisi Viktor Yanukovych na
upinzani unatamka kuundwa kwa serikali ya muungano na kufanyika kwa
uchaguzi wa raisi.
Hata hivyo inabainishwa kuwa watu wengi hususan waandamanaji bado hawana imani na raisi Yanukovych.
Maraisi wa Marekani na Urusi wamekubaliana kuwa mpango huo unapaswa kutekelezwa haraka.
Ikulu ya Marekani imebainisha kuwa Urusi imetaka kuhusika katika mchakato wa utekelezwaji.

0 comments:
Post a Comment