Feb 22, 2014

Ndege ya kijeshi ya Libya yaanguka Tunisia, yauwa 11

Afisa mmoja wa serikali ya Libya na watu wengine kumi wameuawa kufuatia kuanguka ndege moja ya kijeshi karibu na Tunis mji mkuu wa Tunisia.

 Ndege hiyo ilikuwa imebeba wagonjwa. 


Sheikh Meftah Daouadi, Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Mashahidi ya Libya na abiria kumi pamoja na mhudumu mmoja wa ndege wamefariki dunia baada ya ndege hiyo aina ya Antonov kupata ajali wakati ikijaribu kutua.

Shirika la habari la Tunisia limeripoti kuwa ndege hiyo ya Libya ilianguka baada ya rubani kujaribu kutua katika shamba karibu na mji wa Grombalia lililoko umbali wa karibu kilomita 40 kusini mwa Tunis mji mkuu wa Tunisia. 

Tawfik Rahmouni msemaji wa masuala ya ulinzi wa Tunisia amesema kuwa mhudumu wa ndege hiyo ya kijeshi ya Libya aliwasiliana na uwanja wa ndege wa Carthage wa Tunisia kabla ya ajali hiyo akisema kuwa injini za ndege zimeshika moto.

0 comments:

Post a Comment