Rais wa Ukraine, Viktor
Yanukovych amewalaumu viongozi wa upinzani kutokana na vurugu zilizozuka
hivi punde katika mji mkuu Kiev. Katika taarifa, bwana Yanukovych
ametoa wito kwa upinzani kujiepusha na kile alichokitaja kuwa nguvu za
'misimamo mikali'.
Matamshi hayo yanakuja huku mapambano kuhusu mustakabal wa Ukraine yakizuka tena. Baadhi ya waandamanaji wanaoipinga serikali walirusha mawe na mabomu ya petroli kuwashambulia polisi waliokuwa wanawazuia kuandamana hadi makao ya bunge.
Polisi nao walijibu kwa kuwafyatulia risasi za mpira magari ya kutupa maji na maguruneti ya kuwaduwaza waandamanaji hao.
Kila upande unalaumu mwingine kwa kuanzisha mapigano hayo. Vifo vimeripotiwa miongoni mwa waandamanaji na vikosi vya usalama vile vile.
Vurugu hizo zimesitisha shughuli za kawaida katika mji mkuu Kiev kwa majuma kadhaa tagu rais Victor Yanukovych akatae kutia saini mkataba mkubwa wa kibiashara kati ya Ukraine na umoja wa Ulaya na badala yake kutafuta ubia na taifa la Urusi.
Mmoja wa viongozi wakuu wa upinzani Vitali Klitschko amesema mazungumzo na rais Yanukovych yamegonga mwamba baada ya yeye kutaka waandamanaji kuondoka mjini Kiev bila masharti.
"Sina furaha kabisa kwa sababu hayakuwa mazungumzo na rais hataki kusikiza upinzani. Hatawataki kusikiza na njia ya kipekee ni waandamanaji wote kusitisha maandanamano amesema. Lakini kwa sasa ni muhimu kusitisha mapigano," amesema Vitali Klitschko.
Mkuu wa sera za kigeni katika umoja wa Ulaya, Catherine Ashton, amesema ana wasiwasi mkubwa kuhusiana na kukithiri kwa vurugu na kutoa wito kwa wanasiasa kushughulia maswala yaliozua tofauti zilizopo.
Urusi imelaumu wanasiasa kutoka mataifa ya magaribi kwa kuchochea vurugu hizo na badala yake kukatalia mbali kile Moscow inazingatia kuwa vitendo vya kichokozi vya makundi yenye misimamo mikali miongoni mwa waandamanaji.
Ikulu ya White inasema kuwa makamu wa rais wa Marekani Joe Biden amempigia simu rais Yanukovych kumwambia kuwa ana wasiwasi mkubwa kuhusiana na vurugu hizo zinazozidi kuwa mbaya na kumtaka awaondoe wanajeshi wa serikali.
0 comments:
Post a Comment