Feb 26, 2014

UN watahadharisha juu ya hali ya kutisha huko CAR

Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuhusu kushtadi hali mbaya ya kibinadamu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na kuonya juu ya umwagaji mpya wa damu. 

Hayo yanajiri huku Ufaransa ikijipanga kurefusha muda wa kuweko wanajeshi wake nchini humo.
Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeripoti kuwa maelfu ya raia hasa kutoka jamii ya wachache ya Waislamu huko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wanakabiliwa na hatari kubwa ya mashambulizi. 

Adrian Edwards msemaji wa UNHCR ameeleza kuwa zaidi ya watu elfu 15 wengi wao wakiwa ni Waislamu katika maeneo tafauti huko Jamhuri ya Afrika ya Kati hivi sasa wamezingirwa na wanakabiliwa na vitisho vya Wakristo wenye silaha.

Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa pia ametaka kuongezwa wanajeshi wa kulinda amani wa kimataifa na kuimarishwa ulinzi huko Jamhuri ya Afrika ya Kati akisema kuwa misaada ya kibinadamu pekee haitoshi. 

0 comments:

Post a Comment