Feb 13, 2014

Mh,Mansour :msinipe pole kufukuzwa CCM nipeni hongera

Mjumbe wa kamati ya maridhiano Z'bar Mh.Mansour Yussuf Himid akihutubia umma katika mkutano wa hadhara iliofanyika tibirinzi.

Mjumbe wa Kamati ya maridhiano Zanzibar Mh,Mansour Yussuf Himid amesema hivi karibuni alikuwa mwakilishi wa CCM na alifukuzwa kutokana na msimamo wa kudai Zanzibar huru yenye mamlaka yake kamili ambapo jambo hilo lilikuwa tofaut.

Mh,Mansour aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliandaliwa na chama cha wananchi CUF katika kiwanja cha Tibirinzi Chake Chake Pemba siku ya jumapili ya tarehe 9/2/2013 ambapo walialikwa kama wajumbe wa kamati ya maridhiano Zanzibar.

Alisema sula la lutofautiana na wenzake wa CCM ndio kilikuwa chanzo kikubwa cha yeye kufukuzwa ndani ya Chama hicho lakini suala hilo halikumrudisha nyuma kubadili msimamo wake na ndio maana hadi leo hii msimamo wake ni hule hule.

‘’Wananchi msinipe pole kwa kufukuzwa CCM nipeni hongera pengine nimepukana na mengi sana’’alisema Mansour.

Akizungumzia kuhusu uanzishwaji wa mchakato wa katiba mpya,alieleza kuwa muda wote akiwa pamoja na wenzake alikuwa akiwausia kwamba huu ndio muda pekee wa kuikomboa Zanzibar kutokana na muungano huu ambao hauleti usawa kwa wazanzibar,lakini baadhi ya wenzake walikuwa hawaoneshi kumuunga mkono.

‘’Ni muda mrefu sasa wazanzibar tumekuwa tukiunda tume za kukabiliana na kero za muungano lakini hadi sasa hakuna kilichotatuliwa’’alieleza Mansour.

Aidha Mh,Mansour alisema kuwa yeye binafsi hana tatizo na muungano lakini usiwe muungano huu ambao hatoi haki kwa washiriki wawili walioungana badala yake angependa kuona muungano unaotoa usawa kwa washiriki wote.

Wananchi wa Zanzibar hivi ni kweli nyinyi mnaamini kuwa wazanzibar hatuna busara na hekma ya kuamua mambo yetu wenyewe mpaka tukaamuliwe Tanganyika,kufanya hivi nikuwakandamiza wazanzibar wasiwe na uwezo wakuamua mambo yao wenyewe,sasa niwakati pekee wa kuyakataa haya.

Alimtolea mfano Rais wa Zamani wa Taifa la Africa Kusini Mzee Nelson Mandela juu ya kauli yake aliyoitoa inayosema ‘’Uhuru sio kumkata mtu minyororo tu bali ni kuheshimiana kwa kila kitu’’alifafanua Mansour.

Wajumbe kadhaa wa CCM walikuwa wakinipa vitisho kutokana na msimamo wake lakini hakuwa kutishika hata siku moja kwa vile yeye ni mzaliwa wa visiwa hivi vya jamuhuri ya Zanzibar,na hajawahi kuwa mtumwa wao iweje wanilazimishe wanayotaka wao.

Akielezea kuhusu hisia zake katika viongozi mbali mbali wa Nchi hii alisema wazi anampenda sana Maalim Seif Sharif Hamad kutokana na msimamo wake wawazi kwa Wazanzibar na ndio maana amekuwa kivutio kikubwa sana kwa wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

Pamoja na Hayo Mh,Mansour aliwataka wananchi wa kisiwa cha Pemba pamoja na Nchi nzima kwa ujumla kuzidi kumuunga mkono Maalim Seif kutokana na msimamo wake ulio na nia njema kabisa kwa wananchi wote wa Zanzibar na amewaomba wazidi kuwa na subra huenda safari yao ikawa refu kufikia wanapotaka.
Umma mkubwa uliohudhuria Tibirinzi.
Umma mkubwa uliohudhuria Tibirinzi.

0 comments:

Post a Comment