Waislamu wasiopungua 70 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa,
baada ya kundi la Kikristo la Anti Balaka kushambulia kijiji kimoja
kilichopo kusini magharibi mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Taarifa zinasema kuwa, kundi hilo la Kikristo la Anti Balaka lilivamia kijiji cha Guen na kuwalazimisha watu wote kulala chini, kisha kuanza kuwafyatulia risasi na baadhi yao kuwakatakata kwa mapanga na mundu.
Mchungaji Rigobert Dolongo ameviambia vyombo vya habari kwamba mauaji hayo yalikuwa ya kikatili mno.
Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa, mamia ya Waislamu wakazi wa kijiji hicho wameamua kukimbilia kanisani kwa hofu ya kushambuliwa na hata kuuawa na wanamgambo wa Anti Balaka.
Hivi karibuni gazeti la Daily Telegraph la nchini Uingereza liliandika kuwa, makumi ya maelfu ya Waislamu wameshauawa nchini humo, huku maelfu ya wengine wakimbilia nchi jirani.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, hivi karibuni Umoja wa Mataifa uliwataka wanamgambo wa Anti Balaka kuweka chini silaha zao, lakini viongozi wa kundi hilo wamekataa kutii amri hiyo na kusisitiza kwamba wataendeleza mauaji dhidi ya Waislamu nchini humo.

0 comments:
Post a Comment