Feb 25, 2014

Askofu wa Uingereza apandishwa kortini kwa ubakaji

Askofu wa zamani wa Kanisa Katoliki nchini Uingereza jana alifikishwa mahakamani kwa tuhuma za ubakaji, kulawiti na kunajisi watoto waliokuwa chini ya usimamizi wake.
Askofu Francis Paul Cullen mwenye umri wa miaka 85 alikiri mbele ya mahakama katika mji wa Derby kaskazini mwa Uingereza kuwa ametenda makosa 21 ya ubakaji na kuwanajisi watoto wadogo.

Askofu Francis Cullen alipatikana na hatia ya kutenda makosa hayo kuanzia mwaka 1957 hadi 1991, kwa kuwabaka, kuwalawiti  na kuwanajisi wasichana na wavulana wenye umri wa miaka 6 hadi 16 wakati akihudumu kwenye  makanisa mbalimbali ya miji ya Scunthorpe, Leicester, Alfreton,  Debryshire na Machworth. 

Awali askofu huyo alitiwa mbaroni mwaka 1991, na baada ya kufanyika uchunguzi wa awali aliachiliwa huru kwa dhamana. Hata hivyo, askofu huyo hakutekeleza masharti ya dhamana na kuamua kutoroka na kujificha katika mji wa Tenerife nchini Uhispania kwa miongo miwili bila ya kujulikana.
 
Mwezi uliopita, Askofu Francis Cullen alitiwa mbaroni na kurejeshwa nchini Uingereza kujibu tuhuma zilizokuwa zikimkabili. Mahakama ya Uingereza itatangaza hukumu dhidi ya kiongozi huyo wa Kikristo mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment