Askofu Mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, amelaani vikali
mashambulizi ya makundi ya waasi wa Kikristo dhidi ya raia wa Kiislamu
nchini humo.
Dieudonne Nzapalainga ameyasema hayo mjini Bangui katika mazungumzo yake yaliyorushwa hewani na Redio Vatican ambapo mbali na kulaani mashambulizi hayo, amesema kuwa vitendo hivyo vya ukatili vinakinzana na misingi ya dini ya Ukristo.
Nzapalainga ameongeza kuwa, wale wote wanaoshiriki katika mauaji hawawezi kamwe kujiita kuwa ni wafuasi wa dini ya Kikristo.
Askofu mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amesema kuwa, wanachama wa makundi ya waasi wa Anti-Balaka hawawezi kusema kuwa, wanafanya mauaji hayo kwa msingi wa dini hiyo.
Aidha ameyataja mashambulizi ya makundi hayo kuwa ni vita vya kuwania madaraka na kuongeza kama ninavyo mnukuu: “Viongozi wa kiroho, makasisi na mimi mwenyewe, tunasema rasmi kuwa wale wote ambao wanatumia vibaya vijana wa nchi hii kwa ajili ya kutekeleza mashambulizi dhidi ya Waislamu, wanatakiwa kujibu tuhuma dhidi yao katika ngazi za kitaifa na kimataifa,” mwisho wa kunukuu.
Hii ni katika hali ambayo hapo jana Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International lilitangaza kuwa, lina ushahidi unaoonyesha kufanyika mauaji ya mamia ya Waislamu wa nchi hiyo yaliyofanywa na wanamgambo wa Kikristo tangu kulipofanyika mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2013.
Aidha shirika hilo liliongeza kuwa, kuna operesheni za kufukuza jamii ya Waislamu kwa kutumia mauaji katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, suala ambalo askari wa kulinda amani wa kimataifa wameshindwa kulizuia.

0 comments:
Post a Comment