Basi la abiria la Mtei na pikipiki iliyokuwa imebeba
wanafamilia watatu katika mtindo wa mshkaki limeteketea kwa moto na kusababisha kifo cha watu watatu.
Kati ajali hiyo watu wawili walifariki katika eneo la ajali na mwingine kufia njiani wakati anakimbizwa
hospitali.
kwa mujibu wa mashuhuda ni kwamba ajali hiyo iliyotokea saa mbili na nusu Asubuhi katika eneo la minara ya
Posta na TBC mkoani Singida, ilisababishwa na dereva wa pikipiki
alipokuwa akitaka kukata kona bila kuonyesha ishara ya taa wakati basi
la Mtei likiwa linaovateki.
Basi la Mtei lililokuwa limebeba abiria wakati limeanza safari ya
kuelekea Arusha, ililazimu abiria wote kushuka wao na mali zao wakati
wananchi wenye hasira kali walipoamua kujichukulia sharia mkononi kwa
kulichoma basi hilo kama linavyoonekana pichani (chini).


0 comments:
Post a Comment