Jan 11, 2014

Wafaransa wengi wataka majeshi ya nchi yao kuondoka Afrika ya Kati

Wanajeshi wa Ufaransa wakifanya ukaguzi katika kituo cha ukaguzi mjini Bangui
Wanajeshi wa Ufaransa wakifanya ukaguzi katika kituo cha ukaguzi mjini Bangui

Wananchi wengi wa Ufaransa wanaitaka serikali ya nchi yao kuwarudisha nyumbani wanajeshi 1 600 walopelekwa Jamhuri ya Afrika ya Kati kujaribu kudmisha amani, na kuwapokonya silaha wapiganaji wa makundi mbali mbali.
Kufuatana na uchunguzi wa maoni ulochapishwa Jumamosi na taasisi ya IFOP, asili mia 41 tu ya wafaransa wanaounga mkono mpango wa serikali kuwaweka wanajeshi wa Ufaransa huko Jamhuri ya Afrika ya kati, kulingana na asili mia moja 51 walounga mkono mpango huo mwezi mmoja uliyopita.
Mchambuzi wa masuala ya kisiasa mjini Paris Mohamed Swaleh anasema "inavyonekana Wafaransa hawaoni faida ya wanajeshi wa nchi yao kubaki nchini humo, kwa vile hakuna adui mmoja wanaopambana nae, na ni vita vya wenyewe kwa wenyewe. 
 
Zaidi ya Hayo hawajui mapigano yataendelea kwa muda gani kutokana na hali kwamba mapambano yameongezeka".

0 comments:

Post a Comment