KIJANA mwenye umri wa miaka 20 mkazi wa Kijiji cha Isagala, wilayani Kishapu, mkoani Shinyanga, ameuawa na watu waliojichukulia sheria mkononi wakimtuhumu kuiba kuku wanne.
Kijana anayetuhumiwa kuiba kuku, Polisi imemtaja ni Ngaga Shija ambaye alipewa kipigo na kisha mwili wake kuchomwa moto, alikuwa akituhumiwa kuiba kuku hao katika kijiji cha Ikonda.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Evaresti Mangala, kabla ya kifo, Shija alikuwa nje kwa dhamana katika kesi iliyokuwa ikisikilizwa Mahakama ya Wilaya ya Shinyanga, akikabiliwa na mashitaka ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kupatikana na mali ya wizi.
Aliuawa juzi saa 2 asubuhi katika Kijiji cha Isagala Kata ya Mwamashele wilayani Kishapu. Hata hivyo Kamanda alisema mmiliki wa kuku wanaodaiwa kuibwa, hajafahamika.
Alisema usiku wa kuamkia Januari 5, Polisi ilipata taarifa kutoka kwa raia wema juu ya kuwepo na kuonekana kundi la majambazi katika kitongoji cha Ntarechagini Kijiji cha Nyamwaga.







0 comments:
Post a Comment