Dec 22, 2013

Abbas afanya mazungumzo na viongozi wa misri

Rais Mahmoud Abbas wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amekutana na kufanya mzungumzo na Rais Adly Mansour wa serikali ya mpito ya Misri na halikadhalika mkuu wa idara ya kiintelijensia ya nchi hiyo mjini Cairo. 

Kwa mujibu wa ripoti ya Wizara ya mambo ya Nje ya Misri, viongozi hao walijadili kuhusiana na hali ya mabadiliko ya sasa ya Palestina hususan juu ya faili la mazungumzo yanayoitwa eti ya amani kati ya utawala haramu wa Kizayuni na Wapalestina.
Aidha katika mazungumzo hayo, Rais Mahmoud Abbas alielezea nia yake ya kutaka kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa kwa ajili ya kukuza kiwango cha ushirikiano wa pande mbili za Misri na Palestina na hasa kwa kuzingatia nafasi iliyonayo Cairo katika kadhia ya Palestina. 

Abbas amesema kuwa, anataraji katika mustakbali kuiona Misri ikitoa mchango mkubwa katika kutatua migogoro ya kieneo. 

Kwa upande mwingine Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Ofisi ya Kiintelijensia ya nchi hiyo Muhammad al-Tahami na kujadili kuhusiana na hali ya mambo huko Palestina hususan kuhusiana na kadhia ya kuendelezwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika Ukingo wa magharibi wa Mto Jordan na hali ya mambo na matatizo ya watu wa Ukanda wa Gaza.

0 comments:

Post a Comment