HAWA NI BAADHI YA WANA SEMINA.
Wafanya biashara wa kiislamu wamehimizwa kutoa Zaka ili kupata radhi za ALLAH S.W.
Hayo yamesemwa jana katika semina ya ujasiriamali iliyofanyika katika ukumbi wa Istiqama uliopo Ilala Dar es salaam.
Akiwasilisha mada ya Usimamizi wa Biashara,Sheikh Salim Awadh alisema,kumejengeka utamaduni kwa baadhi ya wafanya biashara wa Kiislamu kuiogopa TRA zaidi kiasi cha kukosa amani.
"kimsingi sipingani na kodi hiyo inayokusanywa na TRA lakini wafanya biashara mnatakiwa mumuogope zaidi ALLAH S.W kwa kutoa zakkah kama alivyo amrisha" alisema.
Akitoa mfano alisema "mfanya biashara anayemiliki milioni sabini anatakiwa atoe zaka shilingi laki saba tu,kitu ambacho hakimshindi,lakini cha kusikitisha,mfanya biashara huyu hayupo tayari kutoa kiwango hicho"mwisho wa kumnukuu.
Kwa upande wake katibu mkuu wa Baytul Maal Sheikh Pazi Mwinyimvua alisema "tumeamua kuweka semina hii kwa lengo la kutoa elimu kwa wafanya biashara,kwani somo na lengo la zakkah halifahamiki vizuri kwao"
Naye mkurugenzi wa Baytul maal kutoka TAMPRO Ustaadh Ngoi Kayeko amesema,tafiti zinaonesha asilimia 75 ya wafanya biashara wa Tanzania,biashara zao zinakufa ndani ya miaka mitano tangu kuanzishwa.
Aliongeza kwa kusema "waathirika wakubwa ni wafanya biashara wa kiislamu,ndipo tukaona tuwasaidie kwa kuwapatia semina hizi,japo tuna kabiliwa na changa moto za muitikio hafifu wa wafanya biashara"mwisho wa kumnukuu.
Semina hiyo ya siku moja iliandaliwa kwa ushirikiano wa
HAY ATUL ULAMAA,TAMPRO NA IBNI HAZMI MEDIA CENRTE.
SALIM AWADH AKITOA MADA YA USIMAMIZI WA BIASHARA.
MMOJA WA WAFANYA BIASHARA AKICHANGIA MADA YA USIMAMIZI WA BIASHARA.
HAWA NI BAADHI YA WANA SEMINA.
0 comments:
Post a Comment