Mgomo wa wafanya biashara wa Kariakoo umeshika kasi kwa kuingia siku ya pili.
Mwandishi wa munira blog ilipita katika mitaa mbalimbali na kukuta hali ni mbaya zaidi kuliko jana.
Wakiongea na mwandishi wetu,baadhi ya wafanya biashara hao walisema kama ni mgomo leo ndiyo una komaa na jana ilikuwa ni rasha rasha.
"Unajuwa hii Serikali imezowea kutukandamiza, wametulazimisha tuwe na ving'amuzi baadhi yetu hadi leo TV tumezifunika shuka hatuna uwezo wa kununua ving'amuzi,wakatulazimisha tulipe tozo ya laini za simu tumekubali,leo wanatulazimisha tununue mashune za TRA,kwa hili hatuko tayari nasi tupo tayari kwa lolote".alisema mfanya biashara aliyekataa kutaja jina lake.
Wakati huo huo wafanya biashara hao wameulalamikia Uongozi wao kwa kutowaweka wazi katika mgomo huo unao endelea.
Wamesema "viongozi wetu walituambia watakutana nasi jana saa tano,lakini hawakutokea hadi leo hii tuna watafuta na simu zao zote hazipatikani".Alisema mfanya biashara mmoja ambaye alimpatia mwandishi wetu namba za simu za viongozi
Mwandishi wetu alipompigia mwenyekiti wa wafanya biashara hao kutaka kuthibitisha juu ya muendelezo wa mgomo huo,alisema "mimi siyo mwenyekiti na sifahamu chochote".
SURA HALISI YA MGOMO WA WAFANYA BIASHARA KARIAKOO.
0 comments:
Post a Comment