Naibu mkuu wa usalama wa taifa nchini Libya, Mustafa
Noah, ameachiliwa huru siku moja baada ya kutekwa na watu wasiojulikana
wakiwa na silaha karibu na uwanja wa ndege wa Tripoli.
Mapigano hayo yaliwahusisha wanamgambo na waandamanaji, ambao walikuwa wakijaribu kuwafukuza wanamgambo kutoka mji mkuu Tripoli.
Serikali imekuwa ikijitahidi kuwafukuza wanamgambo hao.
Mgomo wa kutaka wanamgambo waondolewe kutoka Tripoli, umedumu kwa siku tatu.
Waziri Mkuu, Ali Zeidan, alitekwa nyara kwa muda mfupi mwezi uliopita.
0 comments:
Post a Comment