Mfanyabiashara wa magari, Gabriel Munisi (35), jana alijiua
baada ya kumuua mtu mmoja na kujeruhi wengine watatu jijini Dar es
Salaam katika tukio linalohusishwa na wivu wa mapenzi.
Munisi, ambaye alikuwa mkazi wa Mwanza, aliwapiga
risasi watu watatu akiwamo mchumba wake, Christina Alfred katika Mtaa wa
Bungoni Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam.
Baada ya kumpiga risasi mchumba wake huyo na
kudhania kwamba amemuua, inadaiwa kwamba Munisi aliendelea kuwamiminia
risasi watu wengine na kumuua mdogo wake Christina, Alpha (22).
Katika tukio hilo, Christina na mtu anayedaiwa
kuwa mchumba wake mpya, Francis Shumila wamelazwa katika Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili baada ya kujeruhiwa. Mama yake Christina, Helen
Alfred amelazwa katika Hospitali ya Amana baada ya kujeruhiwa pia.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marieta Minangi
alisema Munisi alikutwa na bastola moja, magazini mbili na yalikutwa
maganda 14 ya risasi zilizotumika na risasi mbili ambazo zilikuwa
hazijatumika.
0 comments:
Post a Comment