Kwa mara nyengine tena mgao wa umeme unaanza leo.
Mgao huo utahusisha miji yote mitano nchini huku Zanzibar na mikoa mingine ikionja adha hiyo kwa siku kumi kuanzia leo, hivyo kusababisha adha kwa wakazi wake.
Hayo yamebainishwa na Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania
(Tanesco) Badra Masoud alipokua akieleza
kuwa hali hiyo inatokana na kuzimwa kwa mitambo ya Kampuni ya Pan
African iliyopo Songosongo.
“Mitambo hiyo itazimwa kwa sababu ya matengenezo
ya lazima, hakuna jinsi ya kuzuia hali hiyo Tanesco tunasikitika sana
kwa kuwa kutakuwa na upungufu mkubwa wa umeme kwenye gridi ya taifa,”
alisema Masoud.
Alifafanua mitambo hiyo inaendeshwa na gesi ambayo imepungua katika kisiwa hicho cha Songosongo Wilaya ya Kilwa, Lindi.
“Upungufu huo umesababishwa na matengenezo ya
kiufundi yanayofanywa kwenye visima vya gesi, lengo ni kuboresha
upatikanaji wa gesi ya kutosha kwenye visima hivyo,” alisema.
0 comments:
Post a Comment