Nov 24, 2013

Migogoro Ya Wazazi Ina athiri Elimu Na Maadili Kwa Watoto


MZEE ABDUL AZIZ MUHAMED HASSAN (KUSHOTO) AMBAYE NI MMOJA WA WAGENI RASMI AKIWA NA MWENYEKITI WA BODI YA SHULE BWANA HASSAN AKRABI KATIKA MAHAFALI YA WAKHITIMU WA KIDATO CHA NNE YALIYOFANYIKA JANA SHULENI YEMEN CHANG'OMBE DAR ES SALAAM

Wazazi wametakiwa kuiepuka migogoro baina yao kwani inachangia kudumaza maendeleo ya kielimu kwa watoto.

Wito huo umetolewa jana katika mahafali ya kuwaaga wakhitimu wa kidato cha nne wa shule ya DYCCC Sekondari iliyopo chang’ombe Dar es salaam.
Akiongea katika mahafali hayo,Bwana Abdul Aziz Muhamed Hassan ambaye alikua ni mmoja wa wageni rasmi alisema watoto wanategemea sana ushirikiano na msaada wa hali na mali kutoka kwa wazazi.

Akifafanua zaidi alisema msaada huu wa wazazi hauishii katika kulipa ada tu,bali unaenea katika nyanja mbalimbali ikiwemo kufuatilia maendeleo yao sambamba na kukaa nao kwa lengo la kusikiliza shida zao.

Aidha aliwasihi wazazi kuepuka migogoro na mitafaruku kati yao isiyo ya lazima.

Wazazi wenzangu,ni jambo lisilo epukika katika famila zetu wakati mwengine kuwa na misuguano ya hapa na pale,tahadhari yangu kwenu ni kwamba tuiepuke misuguano hiyo na ikibidi basi misuguano hiyo isiwahusishe watoto”alisema.

Aliendelea kusema kwamba “mitafaruku hii ikiwahusisha watoto itakuwa na nafasi kubwa ya kuathiri maendeleo yao ya kitaaluma na kimaadili”,mwisho wa kunukuu.

Jumla ya wanafunzi 74 wamekhitimu kidato cha nne shuleni hapo,kati hao 45 wakiwa ni wasichana.

Shule ya DYCCC ilimpa heshima ya kuwa mgeni rasmi baada ya mtoto wake (Safia Abdul Aziz) kuwa ni mmoja ya wanafunzi wawili waliofanya vizuri.

 MWENYEKITI WA BODI YA SHULE YA YEMEN HASSAN AKRAB AKIMKABIDHI CHETI MMOJA YA WAKHITIMU WA KIDATO CHA NNE.

 MR ANTIPAS CHALE MKUU WA SHULE YA SEKONDARI YEMEN AKIONGEA KATIKA MAHAFALI HAYO"KUNA DHANA KWAMBA SHULE ZA KIISLAMU ZINA TABIA YA KUFELISHA WANAFUNZI,DHANA HII SI SAHIHI NA TUKISHIRIKIANA TUNA UWEZO WA KUIONDOSHA KABISA"ALISEMA.

 BAADHI YA WAKHITIMU WAVULANA WA KIDATO CHA NNE WAKIWA KATIKA MAHAFALI HAYO.

BAADHI YA WAKHITIMU WASICHANA WAKIWA KATIKA MAHAFALI HAYO JANA.



0 comments:

Post a Comment