Nov 25, 2013

KUKHITIMU KIDATO CHA NNE SIYO MWISHO WA KUJIFUNZA.

 MGENI RASMI SAID SALIM AKIONGEA KATIKA MAHAFALI HAYO.

Vijana wametakiwa kuchangamkia fursa zilizopo katika sekta ya elimu ili kufikia malengo.

Ushauri huo umetolewa hivi karibuni katika mahafali ya tano ya wakhitimu wa kidato cha nne wa shule ya DYCCC Yemen Sekondari iliyopo changombe Jijini Dar es salaam.

Akiongea katika mahafali hayo Mgeni Rasmi Bwana Said Salim Bahyaaq aliwataka wakhitimu hao wafahamu kwamba kidato cha nne si mwisho wa kujifunza bali ni mwanzo wa jitihada za kufikia kilele cha uwezo wao.

Akitumia falsafa pana zenye mvuto alisema,"Wazazi wenu na walimu wenu wanasubiri kwa hamu kubwa kushuhudia mnatoka na mafanikio na mkiweza kutimiza matarajio yao basi mtakuwa mmetimiza malengo yenu"


HAPA MGENI RASMI AKIMKABIDHI MWANAWE (SALIMSAID SALIM) MOJA YA VYETI KWA KUONGOZA JUMLA YA MASOMO 14.

Aliendelea kuwaasa kwa kuwaambia "Ujumbe wangu kwenu vijana ni kwa hali yoyote ile kutosahau lengo lenu la kufikia kilele cha elimu na maarifa kwani hayo ndiyo madhumuni ya hao wanaojitoa mhanga ambao ni wazazi,walezi na wafadhili wenu"Mwisho wa kumnukuu.

Hakusita kuwataka vijana hao wawe na maumivu pindi wanaposhindwa kuyafikia malengo kutokana na matendo ya upuuzi na uzembe.

Bwana Said Salimu alipewa heshima ya kuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo baada ya mtoto wake (Salim Said Salim)  kuibuka mshindi wa jumla kwa kushika nafasi ya kwanza katika mitihani 14.

BAADHI YA VIONGOZI WA BODI YA SHULE YA DYCCC YEMEN NA WAZAZI WAKIFUATILIA KWA MAKINI MATUKIO YALIYOJIRI KATIKA MAHAFALI HAYO.
HAPA WAKHITIMU WAKICHUKUA AHADI MBELE YA MGENI RASMI JUU YA KUTOVUNJA NDOTO ZA KUFIKIA MAFANIKIO.















0 comments:

Post a Comment