Nov 25, 2013

KICHANGA AULIWA.

 Mtoto mchanga ameuliwa na kutupwa dampo.

Akielezea tukio hilo jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minagi, alisema juzi saa 3 asubuhi eneo la Mtoni dampo reline, ilikutwa maiti ya mtoto mchanga wa jinsia ya kike anayekadiriwa kuwa na umri wa siku moja.


Kamanda Marietha alisema maiti hiyo iliyotupwa maeneo hayo na mtu asiyefahamika ilikutwa ndani ya mfuko wa rambo na imehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke huku akisisitiza kwamba hakuna aliyekamatwa. 
INNAA LILLAAH WAINNAA ILAYHI RAAJIUUN

0 comments:

Post a Comment