Sep 7, 2013

TUNAWEZA KULETA MAENDELEO BILA YA KUSUBIRI WAFADHILI.

SHEIKH OMAR AL HAD OMAR


Jamii ya Waislamu wamekumbushwa kwamba wana uwezo wa kuleta maendeleo katika jamii ya Kiislamu bila ya kuwategemea wafadhili.

Hayo yamesemwa jana na Imamu wa Msikiti wa Kichangani Sheikh Omar Al had Omar alipokuwa anawahutubia Waislamu waliofurika katika ibada ya Swala ya jumaa.
Amesema iwapo tutatambua na kuthamini kwamba sisi binaadamu tuna dhamana ya uongozi katika dunia hii,tunaweza kabisa licha ya unyonge wetu huu tukaleta mabadiliko makubwa yenye tija kwa waislamu na jamii kwa ujumla.

Nakubali kabisa kwamba tatizo kubwa ni kwa baadhi ya viongozi kutokuwa na muono wa mbali na wengine kukosa uaminifu,lakini sina shaka na waislamu kwamba wanataka maendeleo ya kweli,sasa hawa waislamu wanaotaka maendeleo ya kweli wakionyeshwa njia yenye usimamizi madhubuti tunaweza kabisa kupata maendeleo bila kutegemea wafadhili”.

"Ndugu zangu Waislamu,leo sisi tumekuwa wahanga wa maendeleo karne kwa karne,Serikali inapotoa huduma haiangalii imani ya watu,bali inatoa huduma kwa kuangalia umuhimu wa huduma,kutokana na hali hiyo sisi tumekuwa na wahanga wa huduma hizo katika sekta mbalimbali,ikiwemo sekta ya afya,na katika sekta hii muathirika mkubwa ni mwanamke wa Kiislamu,leo akitaka kupata huduma ya Utra Sound ni lazima avua nguo na haijalishi anayempatia huduma hii ni mtu wa jinsia gani,hatimaye mwanamke huyu anaipokea huduma hii kwa udhalili mkubwa na kwa unyonge mkubwa,lakini haya yanawezekana kwetu tukaondokana nayo kama tukiwa na mipango madhubuti yenye usimamizi imara”.

Akiongea kwa hisia Sheikh Omar aliendelea kusema”sisi waumini wa masikti wa kichangani tumeliona hilo na tumeamua kwa kila Swala waumini kuchanga shilingi mia mbili ambazo tayari zimeshaanza kuonesha matunda makubwa,tunatoa wito kwenu ndugu zetu mutuunge mkono kwani huu ndiyo wakati wa mabadiliko,tusisubiri mjomba aje kutusaidia”,.

Kufuatia hamasa hiyo munirablog usiku ilimfuata Sheikh Omar nyumbani kwake mtaa wa Uwazani na kufanya mahojiano ya kina na kugundua kwamba ana shehena ya mipango ya maendeleo ambayo kama atapata watu wenye ikhlaswi na moyo wa kujituma jamii ya kiislamu inaweza kutoka katika mnyororo wa fikra tegemezi.

Wakati huo huo,katika hali ya kuunga mkono harakati hizo munirablog itakuwa inatoa takwimu za mapato kwa kila alkhamis sambamba na kufuatilia mchakato mzima wa harakati hizo kwa manufaa ya waislamu

UFUATAO NI MCHNGANUO MFUPI WA MAPATO.

TAREHE
ADHUHUR
SWALA    YA IJUMAA

AL ASRI
MAGHRIB
ISHAA
JUMLA
1
2/9/13
53,000/

101,000
46,000/
50,000
250,000
2
3/9/13
93,000

44,000
61,000/
52,300
250,300/
3
4/9/13


58,000/

82,000/
140,000/
4
5/9/13
85,000/

42,000/
86,000/
50,000/
263,000/