Sep 29, 2013

Tusichupe Mipaka Katika Kutafuta Rizki

 Ustaadh Munawwara Mussa akiwasilisha Mada ya Uchumi katika Mfumo wa Uislamu.

Waislamu nchini wametakiwa kutochupa mipaka katika kutafuta rizki.

Hayo yamesemwa jana na Ustaadhi Munawwara Mussa ambaye ni Mkurugenzi Ustawi wa Jamii wa Baraza Kuu na Jumuiya za Taasisi za Kiislamu Nchini.

Ameyasema hayo alipokuwa anazungumza katika mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa Kiislamu 193 ambao ni Wakhitimu wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Kambangwa iliyopo Kinondoni Jijini Dar es salaam.

Akiwasilisha mada juu ya Mfumo wa Uchumi katika Uislamu Ustaadhi Munawwara alisema mfumo wa uchumi katika uislamu una kanuni zake ambazo waislamu ni lazima wazifuate ili wapate mafanikio.

Akizitaja baadhi ya kanuni hizo alisema "Ndugu zangu wakhitimu,kanuni ya kwanza ni kufahamu kwamba mali zote ni milki ya ALLAH [S.W],hivyo basi kutafuta riziki ni suala la Ibada, ili uweze kuutumikia Uislamu kupitia Uchumi huo"alisema.

"Najuwa kwamba kukhitimu kwenu ni mwanzo wa harakati za kutafuta Rizki,lakini nawaasa Musichupe mipaka katika kutafuta Rizki",mwisho wa kumnukuu.

Ustaadh Munawara hakusita kuelezea masikitiko yake juu ya vijana wengi wanaotamba katika kutafuta riziki kwa njia isiyo halali kuwa ni waislamu pale aliposema "Inasikitisha kuona vijana wa Kiislamu ndiyo wanaongoza kwa kishindo katika miziki ya bongo flavor,taarabu na fani nyengine ambazo ni kinyume na maadili ya Uislamu."

Katika mahafali hayo,mgeni rasmi alikuwa ni Bingwa wa Uchumi Duniani ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Prof Ibrahim Lipumba.

HAWA NI BAADHI YA WAKHITIMU WA KIISLAMU WA KIDATO CHA NNE KATIKA SHULE YA KAMBANGWA

HAWA NI BAADHI YA MABINTI WAKHITIMU WA KIISLAMU WA KIDATO CHA NNE KATIKA SHULE YA KAMBANGWA

BINGWA WA UCHUMI DUNIANI PROFESA IBRAHIM LIPUMBA AMBAYE ALIKUWA NI MGENI RASMI AKISALIMIANA NA AMIR WA WAKHITIMU HAO (KAMUSA)USTAADH MWINYI,MUDA MFUPI BAADA YA KUWASILI KATIKA MAHAFALI HAYO JANA.

KAIMU MKUU WA SHULE WILLIAM SALENDO AKIZUNGUMZA KWA NIABA YA MKUU WA SHULE HIYO KATIKA MAHAFALI HAYO JANA.

MIONGONI MWA WAZAZI AKITUMIA FURSA YA KUWAULIZA MASWALI YA KIDINI WANAFUNZI HAO KATIKA MAHAFALI YALIYOFANYIKA JANA KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA KAMBANGWA

MMOJA YA WANAFUNZI WAALIKWA KUTOKA SHULE YA MANZESE AKIJIBU SWALI.

HUO NI MUONEKANO WA NJE WA SHULE HIYO HAPO JANA.

0 comments:

Post a Comment