Imeelezwa kwamba Dunia imebadilika na wakati tuliopo sasa si ule wakati uliopita.
Hayo yamesemwa na Imamu wa Msikiti wa Kichangani Sheikh Omar Alhad Omar.
Ameyasema hayo leo hii alipokuwa anazungumza na Waumini wa msikiti huo muda mfupi baada ya Swala ya Ijumaa.
Amesema "Kila nyanja imebadilika si ile ya zamani,ukiangalia mfumo wa Biashara,au mfumo wa Elimu na kadhalika umebadilika kwa kiasi kikubwa,kwa bahati mbaya sana sisi Watanzania ndiyo tumekuwa wa mwisho kugundua na kufuata mabadiliko katika kila sekta"
Aliendelea kwa kusema "hata viongozi wanapaswa walijuwe hili,kwamba wanawajibika kuongoza kwa mujibu wa zama tuliyo nayo lakini pia kwa mujibu wa uadilifu,tukio lililotokea kenya wiki iliyopita ni tukio la kujifunza mengi lakini mafunzo moja wapo ni kwamba dunia imebadilika".mwisho wa kumnukuu
Aidha alionyesha masikitiko yake kwa Waislamu wa Tanzania kutokujuwa nafasi yao.
Wakati huo huo michango inayoendelea kuchangwa katika msikiti wa Kichangani imefikia shilingi milioni tano.
Ifuatayo ni Takwimu ya mapato (Tunayo nakala ya mchanganuo huo) tuliyoipata mara baada ya Swala ya Ijumaa leo hii.
Tarehe 13/9/13 420,800/-
Tarehe 14/9/13 63,750 (mchango wa umeme),
Tarehe 15/9/13 115,200/-
Tarehe 16/9/13 141,200/ kuwachangia watoto wanne,
Tarehe 17/9/13 230,000/-
Tarehe 18/9/13 132,000/- (mchango wa umeme),
Tarehe 19/9/13 209,500/-
Tarehe 20/9/13 453,000/-
Tarehe 21/9/13 81,000/-
Tarehe 22/9/13 131,500/-
Tarehe 23/9/13 173,900/-
Tarehe 24/9/13 172,100/-
Tarehe 25/9/13 57,400/-
Tarehe 26/9/13 55,800/-
Jumla ya Pesa yote tangu kuanza kwa michango hiyo September 2 hadi kufika jana tarehe 26/9/13 ni Shilingi 5,422,200
0 comments:
Post a Comment