Vijana wametakiwa kushiriki michezo ya halali ili kuwasaidia kuepuka matendo ya uhalifu.
Wito huo umetolewa jana jioni na waratibu wa ligi ya mpira wa miguu iliyozinduliwa jana katika uwanja wa barafu Magomeni Makuti Jijini Dar es salaam.
Wakiongea na munira blog kwa pamoja waratibu wa ligi hiyo Idd Moshi (Mnyamwezi) ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu ya Yanga na Taifa Star sambamba na Salum Chachili ambaye ni mdau wa Michezo wamesema,wameamua kuanzisha ligi hiyo baada ya kuwaona vijana wengi inapofika jioni wana zagaa uwanjani hapo na kuvuta bangi.
"Unajuwa mwandishi wa habari,uwanja huu miaka ya nyuma ulitumika vizuri sana kulikuwa na ligi mbalimbali,lakini sasa hilo halipo matokeo yake vijana wanazagaa na kuvuta bangi kitu ambacho kwao hakina faida" alisema Idd Moshi.
Aliendelea kusema kwamba "mbali ya matarajio waliyonayo ya ligi hiyo kuonyesha vipaji na hata kuwapatikana ajira kwa vijana hao pia tunaamini itapunguza kama si kuondosha muda wa kutumia dawa za kulevya "mwisho wa kumnukuu.
Kwa upande wake mdau wa michezo Salum Chachili aliipasha munira blog kwamba ligi hii imedhaminiwa na mbunge wa Jimbo la Kinondoni Mhe. Idd Azzan ambaye ndiye aliyechukuwa jukumu la kuandaa zawadi.
Ligi hiyo yenye kuzishirikisha timu nane kutoka mtaa wa Makuti A na Makuti B kata ya magomeni,imezinduliwa jana ambapo mgeni rasmi alikuwa ndugu Semwa Juma ambaye ni mjumbe wa serikali ya mtaa wa makuti A
0 comments:
Post a Comment